IFAHAMU NA UIOMBEE NAFSI YAKO (P



 IFAHAMU NA UIOMBEE NAFSI YAKO (Part 1)


       Bwana Yesu asifiwe,

Ikiwa huwa unaota ndoto hauzikumbuki, ikiwa huwa unaota unajiona uko makaburini au upo kijijini kwenu, ikiwa huwa unaota unakula au unalishwa vyakula... SIMAMA UOMBEE NAFSI SASA

       Ikiwa miguuni kwako huwa unasikia vitu vinatembea au miguu inawaka moto, SIMAMA UOMBEE NAFSI SASA.

     Ikiwa huwa ukianza kuomba akilini(mawazo) yako unapoteza utulivu au unasikia kupiga miayo. Hio ni dalili tosha kuwa nafsi yako imekwamishwa mahali... aseee simama uombe usipuuze.

     Ikiwa unaunapata uvivu wa kusoma Biblia, na ukisoma tu unasinzia.... Asee changamka(stuka) Ombea nafsi sasa.....    

                                  ISAYA 42:22

[22]Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.


                         NAMNA YA KUOMBA:

   Isemeshe nafsi yako kwa kurudia rudia huku ukitumia ZABURI 103:1-6

                              ZABURI 103:1-6

[1]Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. 

Naam, vyote vilivyo ndani yangu 

Vilihimidi jina lake takatifu.

[2]Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, 

Wala usizisahau fadhili zake zote.

[3]Akusamehe maovu yako yote, 

Akuponya magonjwa yako yote,

[4]Aukomboa uhai wako na kaburi, 

Akutia taji ya fadhili na rehema,

[5]Aushibisha mema uzee wako, 

Ujana wako ukarejezwa kama tai;

[6]BWANA ndiye afanyaye mambo ya haki, 

Na hukumu kwa wote wanaoonewa.


                         Pastor Sitta R. Majani

                              +255 692 950 285

                              Prayers Network

                                            &

                                BAWOJ Ministry

Comments