NJIA TATU ZA KUISHINDA DHAMBI NA MAJARIBU

 NJIA 3 ZA KUSHINDA DHAMBI NA MAJARIBU


       Na Pastor Sitta R. Majani.

        +255 692 950 285


     Bwana Yesu asifiwe wapendwa..


        Dhambi imekua ndio mlango mkuu unao mruhusu shetani kuwatawala na kuwatesa Wana Mungu.

       Mahali palipo na dhambi shetani anakua mtawala na mwenye nguvu..


        1 YOHANA 3:8

  *atendaye dhambi ni wa Ibilisi;* kwa kuwa Ibilisi hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihirishwa, ili azivunje kazi za Ibilisi.

        

      👉🏻 Vifungo vingi na mateso walionayo wanadamu, mara nyingi vina mlango wake ambao ni dhambi..  Mahali ambapo pana dhambi uwepo wa Mungu huondoka kwa hio ulinzi unaondoka pia!!  Sasa hapo inakua rahisi shetani  Kuchinja na kuiba na kuharibu kwa kutumiwa magonjwa, vifo n.k


     YOHANA10:10

*Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu;* mimi nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.


     👉🏻Mahali ambapo hapana dhambi shetani hana nguvu (powerless)


         Kwa hio, ili shetani apate uhalali wa kukutesa anachoanza ni kukuletea MAJARIBU yatakayo kupelekea kutenda dhambi. 

      Dhambi ikisha kufarakanisha na Mungu ndipo hata ukiomba msaada, Mungu anakua hakusikii, ndipo adui muovu anapoanza kukutesa


      ISAYA 59:1-2

[1]Tazama, mkono wa BWANA haukupunguka, hata usiweze kuokoa wala sikio lake si zito, hata lisiweze kusikia;


[2]lakini maovu yenu yamewafarikisha ninyi na Mungu wenu, na dhambi zenu zimeuficha uso wake msiuone, hata hataki kusikia.


        *NITASHINDAJE DHAMBI NA MAJARIBU?*


         1. KWA KULISHIKA NENO LA MUNGU (KUJAA NENO)


         2. KWA KUOMBA


         3. KWA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.


        


      1. KWA KULISHIKA NENO LA MUNGU (KUJAA NENO)


       *Zaburi 119:11*

[11]Moyoni mwangu nimeliweka neno lako, 

Nisije nikakutenda dhambi.


          👉🏻 Neno la Mungu linapojaa kiwango cha kutosha ndani ya mtu linanyamazisha na kutisha matendo yote ya mwilini.. Hali ya wakristo wengi kutokushika Neno  la Mungu vya kutosha, imepelekea wengi kuanguka katika dhambi mara la mara..


        👉🏻Hata Bwana Yesu aliyashinda majaribu kule  alikokua akifunga kwa kutumiwa NENO...

           Kila wakati Bwana Yesu alipokua akimjibu shetani alisema imeandikwa..


          2. KWA KUOMBA


     MATHAYO 26:41

    *Kesheni, mwombe, msije mkaingia majaribuni;* roho i radhi, lakini mwili ni dhaifu.


       👉🏻 Usisahau, maombi ni hali ya kupeleka mahitaji yako mbele za Mungu na ni mazungumzo baina yako na Mungu.

        Kitu kingine ninachotaka ujue ni kwamba,  huwezi kuishinda dhambi kwa bidii na akili zako mwenyewe, ingekuwa tunao uwezo wa kuishinda dhambi wenyewe basi Yesu asingekufa msalabani.


     WAEFESO 2:8-9

      [8]Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;


        [9]wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.


       👉🏻 Kwa pointi hiyo basi imetupasa kumuomba Mungu kila wakati ili atuepushe na MAJARIBU kama kwenye sala ya Bwana.


          3. KWA KUJAZWA ROHO MTAKATIFU.


      Moja Kati ya kazi za Roho mtakatifu ndani yetu ni kutuendesha katika kuyatimiza mapenzi ya Mungu na kuishinda dhambi..


      EZEKIELI 36:27

  *Nami nitatia Roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha* katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda.


      Kazi nyingine ya Roho mtakatifu ni kumshuhudia mtu kwa habari ya hukumu na haki na ikitokea mtu ambae ndani yake ana Roho wa Mungu akatenda dhambi, Basi Roho mtakatifu huwa anahuzunika, anaugua na huyu mtu anasikia kuhukumiwa ndani yake na maranyingi mtu huyu huwa anasukumwa kutubu dhambi...


     YOHANA 16:7-8

[7]Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitampeleka kwenu.


[8]Naye akiisha kuja, huyo *atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.*


*2 WAKORINTHO 7:10*

           Maana huzuni iliyo kwa jinsi ya Mungu hufanya toba liletalo wokovu lisilo na majuto; bali huzuni ya dunia hufanya mauti.


           TUBU DHAMBI,. YESU ANARUDI KULINYAKUA KANISA LA KWELI.


            PASTOR SITTA R. MAJANI

                +255 692 950 285

               PRAYERS NETWORK

                                & 

               BAWOJ MINISTRIES 

Comments