NITAFANYAJE IKIWA NIMEOKOKA LAKINI MAISHA YANGU HAYANA FURAHA NA AMANI.
Na Pastor Sitta Majani..
Bwana Yesu apewe sifa, kumekua na hali ya wapendwa wengi Sana kupita katika hali ya kukosa furaha kwenye MAISHA yao ingawa wengi wao wamempokea Yesu...
Changa Moto hizi zinaweza kuwa,
1. Kwenye huduma.
2. Kwenye ndoa
3. Ofisini na kwenye maeneo ya uchumi
Hali hii inaweza isihusiane na hasara au ugonjwa. Isipokua kunakua na hali ya uzito, uchovu au kutokufurahia aina ya maisha ulioyachagua ikiwa ni pamoja na maeneo matatu niliyoyataja hapo juu....
Nasema hivi unaweza ukawa una kazi nzuri, inakulipa vizuri, hauna hasara lakini haujawahi kuwa na furaha nayo, husikii muamko wa ndani wa kuendelea na kazi, yaani unafanya kwa kujisukuma tu... Au wakati mwingine unajituma Sana kazini lakini unapoteza furaha bila sababu za msingi
Au unaweza kuwa UMEOKOKA na unahuduma na inakwenda vizuri tu, lakini ndani yako hauna furaha wala amani, yaani huenjoy kabisa, unafanya Kama kutimiza wajibu tu, na wakati mwingine mpaka usukumwe sukumwe... Yaani hauifurahii kabisa huduma yako na haikuletei amani Kama mwanzo....
Unaweza pia ukawa uko ndani ya ndoa, mkeo au mumeo ni mwaminifu kwako saana tu, hata wewe unajua hilo, tena zamani ulimfurahia Sana akiwa karibu nawe, lakini Ghafla huna furaha nae, unaanza kusikia hali ya kuto kumfurahia tena bila sababu kabisaaa!!!
UKIONA HALI HIO UFANYEJE...?
1. Uite ufalme wa Mungu ujekwenye eneo lililo na migogoro hio.
WARUMI 14:17
Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni *haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.*
👉🏻 UKIONA kwenye eneo mojawapo kunakosekana HAKI, AMANI, FURAHA Basi ujue kuwa mahali hapo UFALME WA MUNGU haupo ..
Kila penye ufalme wa Mungu, lazima pawe na Haki, Amani na Furaha...... Ukiona linapungua jambo hata mojawapo... Amka, changamka uombe ili ufalme wa Mungu uje kwenye eneo hilo..
Yawezekana nimekuchanganya kidogo, wengi wenu mnajiuliza, inawezekanaje ufalme wa Mungu utoke mbinguni uje duniani!!!?
Mpendwa hata kwenye Sala ya Bwana Kuna mahali tunaomba Ufalme wa Mungu uje(ufike) litakalofanyika hapa duniani Kama huko mbinguni...
MATHAYO 6:9
Mpendwa unapookoka palepale unafanyika kuwa raia wa mbinguni anaeishi duniani, kwa hio unaanza kuoparate katika utawala wa kimbingu, tangu ukiwa duniani.
Ni wajibu wako kuuita ufalme wa Mungu hapa duniani .. Nasema hivi, ukiokoka unaanza kuonja raha ya utawala wa mbinguni ukiwa bado duniani..
Mpendwa unachotakiwa kujua, ukishaokoka tu, Unafanywa kuwa uzao wa *Kifalme na kikuhani*
KUTOKA 19:5-6
[5]Sasa basi ikiwa mtaitii sauti yangu kweli kweli, na kulishika agano langu, hapo ndipo mtakapokuwa tunu kwangu kuliko makabila yote ya watu; maana dunia yote pia ni mali yangu,
[6]nanyi mtakuwa kwangu UFALME WA MAKUHANI , na taifa takatifu. Hayo ndiyo maneno utakayowaambia wana wa Israeli.
UFUNUO 1:5-6
[5]tena zitokazo kwa Yesu Kristo, shahidi aliye mwaminifu, mzaliwa wa kwanza wa waliokufa, na mkuu wa wafalme wa dunia. Yeye atupendaye na kutuosha dhambi zetu katika damu yake,
[6]na kutufanya kuwa UFALME na MAKUHANI kwa Mungu, naye ni Baba yake; utukufu na ukuu una Yeye hata milele na milele. Amina.
👉🏻 Mpendwa ikiwa wewe umemwamini Yesu na ukafanyika kuwa mfalme na kuhani, inakuwaje unapoteza haki zako ofisini,. Ni mfalme yupi anaekosa haki zake!!?
Ukiona hivo, Basi ujue hauzijui haki zako.... Fanya haraka kuuita Ufalme wa Mungu hapo ili haki zako zionekane...
2.Mtegemee na umwamini Roho mtakatifu
Walokole wengi wa leo hawampi nafasi Roho mtakatifu, hawaoni Kama ni wathamani katika wokovu wao... Wengi wamesahau Kama Roho mtakatifu ndie Alie kabidhiwa kanisa Hadi Yesu atakaporudi...
Mpendwahata ukisoma ma vizuri kwenye WARUMI 14:17
inasema,
_Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu
Mpendwa,
Haki, Amani na Furaha vyote viko ndani ya Roho mtakatifu
Ndio maana hata kwenye tunda la Roho utakuta furaha na amani vinatajwa kama tunda la Roho...
WAGALATIA 5:22
Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha , amani , uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu,
NB. UKIONA MAHALI UPO NA HAPANA HAKI FURAHA NA AMANI BASI UJUE HAPO MUNGU HAYUPO...ALIPO MUNGU PANA AMANI, ALIPO MUNGU PANA FURAHA, ALIPO MUNGU HAPANA UENEVU BALI PANA HAKI...
Fanya Maombi ya kurejesha Ufalme wa Mungu.. muombe Roho mtakatifu atawale,Huduma yako, ndoa yako, masomo yako n.k
PASTOR Sitta R Majani
+255 692 950 285
Prayers Network
&

Comments
Post a Comment