MAJIBU YA MAOMBI YANGU YAMECHELEWA JE, NIFANYEJE?


MAJIBU YA MAOMBI YANGU YAMECHELEWA JE, NIFANYEJE?

*PART 1


Na Pastor Sitta R. Majani

 +255 692 950 285


Karibu sana katika somo zuri ambalo litakufanya ujue cha kufanya kabla haujaomba ili uwe katika nafasi ya kujibiwa maombi yako haraka..


ANGALIZO

         Somo hili ni kwa kila aliyemfanya Yesu kuwa Bwana na mwokozi wamaisha yake, kama bado haujaokoka au haujaimarisha mahusiano yako na Mungu tafadhali, anza kwanza kuweka mahusiano yako na Mungu kwa njia ya kumuamini Yesu, kwani utakatifu ni jambo la lazima na  Mungu hasikilizi maombi 

              YOHANA 9:31

[31]Twajua ya kuwa Mungu hawasikii wenye dhambi; bali mtu akiwa ni mcha Mungu, na kuyafanya mapenzi yake, humsikia huyo


MAMBO MUHIMU YANOYOMFANYA MUNGU KUTOA MAJIBU AU BARAKA KWA HARAKA


        1. MAONO AU MATAZAMIO (VISION)

Maono ninayoyamaanisha hapa ni malengo, matazamion, ni ile hali ya kuitazama kesho yako..


                             MITHALI 29:18

    [18]Pasipo maono, watu huacha kujizuia; Bali ana heri mtu yule aishikaye sheria.


👉🏻 Mwandishi wa mithali hapa alikua anamaanisha kuwa mtu akiwa  hana maono juu ya jambo lolote ana weza kufanya lolote bila kujizua kwa sababu  hana maono ya kesho yake.. 


Mfano; 

        Mtu yoyote asie kuwa na matazamio au maono ya kesho yake anaweza kuwa na maisha ya kutapanya mali kwa ulevi na uasherati hii yote ni kwa sababu hana maono..

      Kwa mantiki hio basi, Mungu nae  hawezi kuachilia baraka zake kwa mtu asiekua na maono. Kunawatu wanaomba saana lakini hawajawa na maono (vision ) juu ya kile wanacho kiomba… ndugu zangu Mungu  wetu sio Mungu wa kutaka Hasara,  hawezi  kukupa kitu halafu kipotee tu.  Yeye mwenyewe nasema ndie atufundishae kupata faida 


ISAYA 48:17

         [17]BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni. BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata.


     👉🏻Wapendwa Mungu wetu sio Mungu wa hasara, anataka kuona anapokupa Baraka zake , hazipotei.. ndio maana kabla hajaachilia majibu yake kwako anataka kuona unaona nini/unatazamia nini, nini unacho kiona mbele yako..

👉🏻Wakati mwingine Mungu mwenyewe huanza kukuonesha maono kabla haja kupa kile anataka kukupa, naweza kusema Mungu anakupa kwa kadiri ya unachokiona.. 


      MWANZO 15:5-6

    [5]Akamleta nje, akasema, Tazama sasa mbinguni, kazihesabu nyota, kama ukiweza kuzihesabu. Akamwambia, Ndivyo utakavyokuwa uzao wako.

[6]Akamwamini BWANA, naye akamhesabia jambo hili kuwa haki.


👉🏻Hapa Mungu alikua anamtazamisha Ibrahim maono juu ya baraka za uzao wake zitakavyokua ili kumfanya Ibrahim awe na Imani juu ya ahadi za baraka zake.. 

Shida ya waombaji wengi huwa wanaomba baraka za Mungu bila kuwa na maono, kwasababu maono huwa yanakawaida ya kumuandaa mtu kabla hajapata anacho kitarajia..


  Mfano;

       Wazazi wenye maono  ya kuwa na watoto, huwa wanaweka akiba ya mali kwa ajili ya watoto wanao watarajia hata kama hawajawapata.

    👉🏻Unakuta dada anamuomba Mungu ampe mume bora mcha Mungu lakinini yeye hajajiweka tayari kuwa mke bora, unakuta bado anamaisha ya starehe, hajajiandaa kushi kwa kumnyenyekea mwanaume… kitendo cha kutokujiandaa ni hali ya kutokua na maono.

     👉🏻Unakuta mtu kamaliza kuomba Mungu halafu bado anasema eti “hata sijui itakuwaje” 

Yaani kweli unaomba mpaka unamaliza bado hujui itakuwaje? 

👉🏻Swali langu kwako mkristo, huwa naona nini kabla na baada ya kuomba?..

      Hata Bwana Mungu aliwauliza watumishi wake kadhaa kabla hajaachilia Baraka


YEREMIA 24:3-5

          [3]Ndipo BWANA akaniambia, Unaona nini Yeremia? Nikasema, Naona tini; tini nzuri zilizo nzuri sana; na tini mbovu zilizo mbovu sana, zisizoweza kuliwa, kwa kuwa ni mbovu sana.

[4]Kisha neno la BWANA likanijia, kusema,

[5]BWANA, Mungu wa Israeli, asema hivi, Kama zilivyo tini hizi nzuri, ndivyo nitakavyowaangalia mateka wa Yuda, *niliowatoa katika mahali hapa, waende mpaka nchi ya Wakaldayo, wapate mema.


AMOSI 8:2

          [2] Akaniambia, Amosi, unaona nini? Nikasema, Naona kikapu cha matunda ya wakati wa hari. Ndipo BWANA akaniambia, Mwisho wao umewajilia watu wangu Israeli; sitawapita tena kamwe

 [6]Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi.


ZEKARIA 4:2-6

       [2 ] AKANIULIZA, UNAONA NINI?   Nikasema, Nimeona, na tazama, kinara cha taa cha dhahabu tupu, nacho kina bakuli juu yake, na taa zake saba juu yake; tena iko mirija saba ya kuleta mafuta, kwa taa zote zilizo juu yake;

[3]na mizeituni miwili karibu yake, mmoja upande wa kuume walile bakuli, na mmoja upande wake wa kushoto.

[4]Nami nikajibu, nikamwambia yule malaika aliyesema nami, nikasema, Ee Bwana wangu, vitu hivi ni nini?

[5]Ndipo malaika aliyesema nami akajibu, akaniambia, Hujui vitu hivi ni nini? Nikasema, La, Bwana wangu. 

[6]Akajibu akaniambia, akisema, Hili ndilo neno la BWANA kwa Zerubabeli, kusema, SI KWA UWEZO, WALA SI KWA NGUVU, BALI NI KWA ROHO YANGU, ASEMA BWANA WA MAJESHI.

👉🏻Je, unaona nini? Unaona ushindi au unaona kushindwa,  Maono ni muhimu sana kwenye maombi… maana Mungu wetu anatamani tutazame mbele nay eye yuko tayari kutufunulia ya mbele.





Mtu asie na maono hana tofauti na mtoto anaeanza shule darasa la kwanza anaweza kuifurahia shule lakini hajui kwa nini yuko shule. Ikitokea mtoto huyu kachapwa na mwalimu wake,  basi hata shule yenyewe atakua  hataki kwenda tena , maana hana maono yoyote juu ya yeye kuwepo shule.


      TABIA ZA WATU WASIOKUA NA MAONO

1.Ni watu walio dumaa

2.Ni watu wasio na maandalizi

3. Ni watu ambao hata wa kipata wanatapanya haweki akiba ya kesho yao.

4. Ni watu wanaoishi kwa mashaka, hawana uhakika na kesho yao

5. Ni watu wasiotaka kuzalisha kwa ajili ya kesho  yao.


  Somo litaendelea...


                        PASTOR SITTA R. MAJANI

                               +255 692 950 285

                             PRAYERS NETWORK

                             BAWOJ MINISTRIES 

Comments