IFAHAMU NA UIOMBEE NAFSI YAKO (PART 3)





IFAHAMU NA UIOMBEE NAFSI YAKO (PART 3)

           KUMTENGENEZEA MUNGU NAFASI (MAHALI PAKUKAA)

          Bwana Yesu asifiwe wana wa nuruni, 

       Ni kwa Muda sasa tumekua tukimuomba Mungu aende nasi(atembee nasi), lakini umeshawahi kujiuliza ukitembea na Mungu atakaa wapi ikiwa haujamtengenezea mahali pakukaa?

   Wapendwa wangu, Mungu anapotaka kuweka makazi mahali popote ni lazima pawe na madhabahu. Kwa kifupi ni kwamba, Mungu hukaa katika madhabahu

    Swali langu ni je, umejiandaaje ili uwe madhabahu inayotembea? 

     Wapendwa, ni kweli kabisa Yesu mwenyewe anatamani kukaa ndani yetu, tena mara bilioni zaidi kuliko sisi tunavotamani awe ndani Yetu, ndio maana anabisha hodi.

      UFUNUO 3:20

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami.

 

         YOHANA 15:4-5

[4]Kaeni ndani yangu, nami ndani yenu. Kama vile tawi lisivyoweza kuzaa peke yake, lisipokaa ndani ya mzabibu; kadhalika nanyi, msipokaa ndani yangu.

[5]Mimi ni mzabibu; ninyi ni matawi, akaaye ndani yangu nami ndani yake, huyo huzaa sana; maana pasipo mimi ninyi hamwezi kufanya neno lo lote.

        

         Mpendwa, umeanadaa nafasi moyoni(nafsini) mwako ili huyu Mungu wetu apate kukaa pamoja nawe? 

   Au na wewe umeishia kuomba Mungu akae nawe wakati umemfungia mlango asiingie ndani yako?

       Au hamjui kuwa ninyi ni hekalu la Mungu alie hai?

       1 WAKORINTHO 6:19

       Au hamjui ya kuwa mwili wenu ni hekalu la Roho Mtakatifu aliye ndani yenu, mliyepewa na Mungu? Wala ninyi si mali yenu wenyewe;


       Nugu zangu, asilimia kubwa ya wapendwa wamekua wakiomba kwa machozi na kwikwi wakimuomba Mungu kwa kusema *usinipite mwokozi.* lakini Yesu akitaka kuingia anakuta hakuna nafasi ya kukaa yeye.

Imepelekea hadi wengine wanahisi labda Mungu anaupendeleo.


      Sikiliza rafiki, hata watu wa upande wa giza wanapotaka kutembea na mizimu yao(miungu),  huwa wananyamazisha vipaumbele vyao na wanakubali kuongozwa na miungu .. 

        Nasema hivi mara nyingi miungu inapotaka kuweka maskani ndani ya mtu huwa inataka yule mtu aishi kama itakavyo ile miungu, sio mtu aishi atakavyo... 

       Ikitokea akaishi atakavyo ndio utasikia "amekiuka miiko mizimu ikamuacha au ikamuadhibu"

       Na maranyingi hawa watu kunabaadhi ya vyakula wanakatazwa wasile, baadhi ya mavazi wanazuiwa kuvaa.. ilimradi tu ile miungu ikae itakavyo?

      👉Sasa swali langu kwako mpendwa ni; Je, umejiandaa kuishi kama Mungu atakavyo au kama wewe utakavyo?

      Ukitaka Mungu atembee na wewe, uishi kama Mungu atakavyo, sio utakavyo wewe... yaani ujikane mwenyewe (uviweke pembeni vipaumbele vyako).. Uwe tayari kubeba kusudi la Yesu.

            LUKA 9:23

    Akawaambia wote, Mtu ye yote akitaka kunifuata, na ajikane mwenyewe, ajitwike msalaba wake kila siku, anifuate.


               NINAWEZAJE KUMTENGENEZEA MUNGU MAKAO NAFSINI (MOYONI) MWANGU?


       Mpendwa ni lazima tumtengenezee Muungu wetu mazingira mazuri ya kukaa nasi, vinginevyo hawezi kukuaa nasi... 

     Ndio maana Mungu alipotaka kukaa na wana wa Izrael alimwambia Musa atengeneze sanduku la agano ili akae nao... 


         KUTOKA 25:8

[8]Nao na wanifanyie patakatifu; ili nipate kukaa kati yao.


      Hata wewe ni lazima utengeneze mahali pa Mungu kukaa...


          1.  MAWAZO/ FIKRA/TAFAKARI.

    Mawazo na fikra ni zao la nafsi... 

     Ukitaka kujua kama Mungu ananafasi ndani yako, anza kujichunguza asilimia ya mawazo yako, ni kitu gani unachowaza sana... 

      Kile unacho kiwaza sana sana ndicho kilichojaza nafsi yako... 

      Fundisha nafsi yako kutafakari mambo ya Mungu Muda mwingi, anza kwa kuilazimisha hatimae utaanza kusikia raha unapotafakari mambo ya Mungu na ndipo Mungu anachukua nafasi katika moyo wako..

     👉Unaempenda utamuwaza maranyingi, huwezi kusema unampenda Mungu wakati hata kumuwaza humuwazi... 

    👉Mpe Mungu nafasi ndani yako kwa njia ya kumuwaza (tafakari)sanaa (meditation)...!!

      ZABURI 119:48

   Na mikono yangu nitayainulia maagizo yako niliyoyapenda, Nami nitazitafakari* amri zako.


       ZABURI 63:6

[6]Ninapokukumbuka kitandani mwangu, Nakutafakari Wewe makesha yote ya usiku.


              ZABURI 119:27

[27]Unifahamishe njia ya mausia yako, Nami nitayatafakari maajabu yako.

    

       ZABURI 107:43

[43]Aliye na hekima na ayaangalie hayo; Na wazitafakari fadhili za BWANA.


            Pastor Sitta R Majani

           +255 692 950 285

             Prayers Network

            &

              BAWOJ Ministries 

Comments