IFAHAMU NA UIOMBEE NAFSI YAKO
Part 2
Bwana Yesu asifiwe!!..
NAFSI NI NINI?
👉Nafsi ni utu wa ndani uliobeba utashi, mawazo, fikra, tafakari n.k
Pia nafsi imeandikwa kama moyo katika biblia
👉Nafsi ndio kiunganishi cha roho ya mtu na mwili wake.. Nafsi imetokana na roho na mwili wa mtu kukutana, yaani Mungu alipopulizia pumzi ya uhai(roho) kwenye mwili wa mtu, palepale nafsi nayo ikaumbika.
MWANZO2:7
BWANA Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai.
👉Wachawi na ulimwengu wa giza wanapotaka kumtesa mtu, huwa hawagusi mwili au roho yake, wao wanashughulikia nafsi tu..
Utashangaa unaanza kuchukia Ibada au hutaki kabisa kusoma Neno, unadhani nihali ya kawaida kumbe wameshika ufahamu kupitia nafsi yako.
Hata ukiimba mawazo yako yanahamishwa, unajikuta unachoimba nitofauti kabisa na unachowaza, au unaomba lakini unaishia kuomba mdomoni lakini mawazo yako yanatanga tanga huku na kule....!!
Mpendwa hali ya kuhamishwa mawazo kwenye ibada, Neno au maombi, sio hali ya kawaida... Ni vita, shetani anaogopa sana anapoona unachokisema na kukitafakari muda huohuo..!! Ndio maana wanashika fikra zako na ufahamu kwa njia ya nafsi... uli ujikute unaomba kwa mdomo tu bila kujenga picha kichwani.
MATHAYO 15:8
Watu hawa huniheshimu kwa midomo; Ila mioyo yao iko mbali nami.
NAMNA YA KUOMBEA NAFSI..
1. Omba rehema kwa Mungu juu ya kutoifundisha nafsi yako kupenda cha Mungu..
2. Omba rehema kwa ajili ya sadaka zilizotolewa ili kuingiza nafsi yako katika maagano ya miungu.
MATHAYO 6:21
[21]kwa kuwa hazina yako ilipo, ndipo utakapokuwapo na moyo wako.
3. Tenganisha nafsi yako na watu uliowahi kushirikiana nao mambo kama unzinzi, sadaka za agano, Viapo vya kutokutengana, viapo vya damu n.k
1 WAKORINTHO 6:16
Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.
4. Muombe Mungu akuumbie nafsi(moyo) yenye kumpenda na kumpendeza... ikiwezekana lia mbele za Mungu, omba kwa kubembeleza aubadili moyo wako(nafsi)..
ZABURI51:10
Ee Mungu, uniumbie moyo safi, Uifanye upya roho iliyotulia ndani yangu
5. (A)Kemea kuzimu iliokamata nafs yako, amuru miungu ya kabila na ukoo wenu ikuachie kwa jina la Yesu...
(B) Haribu sadaka za damu zilizoachiliwa ili kukuunga nafsi yako na miungu....
(C) Komboa kitovu chako,nywele zako za utotoni, kwajina la Yesu.
( D) Teketeza kwa moto wa Roho mtakatifu nguo na viatu ulivorithi kutoka kwa marehemu yeyote na kila kitu ulichopokea kama zawadi.... na ujitenge na hizo roho.
(F) Komboa kwa damu ya Yesu pesa za msaada, vitu na sadaka zako zote ulizotoa kwa watu nje. ya uwepo wa Mungu.
(G) Ita kwa nguvu (Amuru) nafsi yako irudi kwenye mwili wako kwa jina la Yesu huku ukitumia mstari wa
ISAYA 42:22
[22]Lakini watu hawa ni watu walioibiwa na kutekwa; wote wamenaswa katika mashimo, wamefichwa katika magereza; wamekuwa mawindo, wala hapana aokoaye; wamekuwa mateka, wala hapana asemaye, Rudisha.
Mungu aingilie kati katika vita hii ya kiroho kwa jina la Yesu.
Pastor Sitta R. Majani
+255 692 950 285
Prayers Network
&
BAWOJ Ministries

Comments
Post a Comment